1 Samweli: 16:6-10 - Walipofika, Samweli akamwona Eliabu naye akafikiri, “Hakika mpakwa mafuta wa BWANA anasimama hapa mbele za BWANA. ” Lakini BWANA akamwambia Samweli, “Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. BWANA hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini BWANA hutazama moyoni. Kisha Yese akamwita Abinadabu na kumpitisha mbele ya Samweli. Lakini Samweli akasema, “Hata huyu BWANA hakumchagua. ” Kisha Yese akampitisha Shama, lakini Samweli akasema, “Wala huyu BWANA hakumchagua. ” Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, “BWANA hajawachagua hawa. ”
Katika hadithi hii nabii Samweli alimtembelea Yese, mwanainchi wa Bethelehemu, kutia mafuta badhi ya mojawapo wa wana wake kama mfalme Bwana alimtuma pale, lakini hakumwambia mapema mwana yupi angemchagua. Yese alifuata mila za wakati huo – alianda karamu kwa mgeni wake wa heshima (Nabii) na kuruhusu watoto wake kupita mbele zake moja baada ya mwengine, akianza na mukubwa. Kama njia ya kuwatambulisha kwa mtu wa Mungu inaonekana hakuna yeyote aliyejua lakini Samweli sababu ya yeye kuwa pale. Hata wanabii hufanya makosa katika njia yao ya kuwaza hii ndio sababu tuna muliza Bwana kuhusu kila kitu. Nabii Samueli alitazama kwa mwana wa kwanza na akafikiria alionekana kana mfalme na ilibidi Mungu kumrekebisha. Mungu hukataa wana wazaliwa wa kwanza kwa sababu Bwana hangali vitu ambavyo mtu hudhamini Bwana hutazama kwa moyo. Mwanadamu huangalia kwa nje. Hawa ndugu halijiunga na Daudi, wakati alikuwa anamtorokea. Saulo, lakini katika wakati huu na hili hadithi wako bado kwa mapishano pamoja na yeye. Ujumbe huu unatupatia majina matatu ya wana hawa. Bwana anatupa somo katika hawa ndugu watatu ambao majina yao yako hapa chini.